2 Chronicles 9:29-31

29 aKwa habari za matukio mengine ya utawala wa Sulemani, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati? 30 bSulemani alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 31 cKisha Sulemani akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Copyright information for SwhKC